SOMO: MACHUKIZO NDANI YA NYUMBA YA MUNGU
(YEREMIA 32:33-34)
“Tena wamenigeuzia visogo vyao, wala si nyuso zao; ingawa
naliwafundisha, nikiondoka mapema na kuwafundisha, lakini hawakusikiliza
ili wapate mafundisho. Bali waliweka machukizo yao ndani ya nyumba
iliyoitwa kwa jina langu, ili kuinajisi”.
Machukizo ya aina yoyote hayaruhusiwi ndani ya nyumba ya Mungu na ndani ya nyumba zetu.
( KUMBUKUMBU LA TORATI 7:26 )
“na machukizo usitie ndani ya nyumba yako, usije wewe kuwa kitu cha
haramu mfano wake; ukichukie kabisa, na kukikataa kabisa; kwa kuwa ni
kitu kilichoharamishwa”.
Machukizo yanatajwa kuwa ni kitu kilichoharimishwa. Neno machukizo
linatokana na neno la lugha ya kiebrania linaloitwa” toebah”. Neno
“TOEBAH” lina maana ya kitu au mtu ambaye ni wa tofauti katika hali. Mtu
ambaye ni hatari ukilinganisha na watu wengine. Yatakuwa ni mambo au
tabia ambazo ziko kinyume na asili yake.
Machukizo sasa ni vitu vya kipagani ambavyo vimeingia ndani ya nyumba ya
Mungu. Yapo mambo ambayo ni machukizo ndani ya nyumba ya Mungu. Mambo
ambayo ni haramu kuingizwa ndani ya nyumba ya Mungu.
( i ). Mwanamke kuvaa mavazi ya wanume na mwanamume kuvaa mavazi ya wanawake.
( KUMBUKUMBU LA TORATI 22:5 ). ‘ Mwanamke asivae mavazi yampasayo
mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila
afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako”.
Mungu anasema maumbile yetu ndiyo yatufundisheni vazi lipi linafaa
kuvaliwa na wanaume na ni nlipi linafaa kuvaliwa na wanawake ( 1
WAKORINTHO 11:14 ). Mitindo ya ushonaji nguo iadizainiwa kutokana na
maumbile yetu. Ndiyo maana wanawake wana mavazi yao na wanaume wana
mavazi yao na Mungu ameliweke hilo mwenyewe. Kwa hiyo vazi kama suruali
siyo la mwanamke, limedizainiwa kwa ajili ya mwanamume na si vinginevyo.
Katika biblia ni wanaume pekee wanaotajwa wakiwa wamevaa suruali,
hatuoni sehemu yoyote ikimtaja mwanamke akiwa amevaa suruali.
Ingia katika blog yangu ujifunze somo la “MAVAZI YA KIKAHABA” utajifunza mengi kuhusiana na mavazi. WWW.davidcarol719.wordpress.com
Suruali kwa wanawake ni vazi la kikahaba kabisa ( MITHALI 7:10 )
( ii ). Sadaka ya kahaba na Mbwa ni machukizo mbele za Mungu
( KUMBUKUMBU LA TORATI 23:18 )
“Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya BWANA,
Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo
kwaBWANA, Mungu wako yote mawili”. Mbwa ni mtu anayerawiti au mtu
anayerawitiwa. Mshahara wa kahaba na watu wote wanaoshiriki katika
uchafu wa kurawiti na kurawitiwa ni machukizo kwa BWANA, Mungu wetu.
Hatutakiwi kupokea sadaka zao kwa ajili ya BWANA, ni machukizo kwake.
( iii ). Miungu na chochote kinachohusiana na miungu ni machukizo mbele za Mungu.
( EZEKIELI 8:1-18 )
Namna yoyote ya sanamu tunapoihusisha katika ibada tayari inakuwa ni
ibada ya miungu. Mapambo ya aina yoyote ni chukizo mbele za Mungu wetu
kwa sababu kuna uhusiano kati ya mapambo na miungu. Ni muhimu kufahamu
kuwa mapambo hayakuvaliwa na Waisraeli. ( WAAMUZI 8:24 ) “ Kisha Gideoni
akawaambia, Mimi nina haja yangu kwenu, ni yakila mtu kunipa hizo
pete za masikio ya mateka yake. ( Kwa maana walikuwa na pete za masikio
za dhahabu, kwa sababu walikuwa ni Waishmaeli )”. Waishmaeli walikuwa ni
wapagani ( mataifa ) vilele waliitwa Wamidiani.
( MWANZO 35:1-4 ).
“……………Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake na wote waliokuwa pamoja
naye, Ondoeni miungu migeni iliyoko kwenu,………..Nao wakampa Yakobo,
miungu migeni yote iliyokuwa masikioni mwao, na pete zilizokuwa
masikioni mwao…………….”.
Mwanamke Yezebeli alikuwa mataifa tena mwabudu miungu. Mwanamke
huyo alikuwa staid sana kwa kujipamba na aliingia katika Taifa la
Israeli baada ya kuolewa na mfalmeAhabu. Kwa hiyo mapambo yalikuwa
yakivaliwa na Waisraeli kwa kuiga tabia za mataifa
( 2 WAFALME 9:30-37; UFUNUO 2:20 )
Makanisa mengi leo yanahudu mafundisho ya Yezebeli ya kuruhusu mapambo
kwa watu wa Mungu. Mungu aliwatumia mitume kwa ishara na miujiza mikubwa
kutokana na injili yao kuwa kinyume na machukizo. Kanisa la kwanza
walifundishwa kuwa mbali na mapambo ya kila namna ( 1 TIMOTHEO 2:9-10;
1PETRO 3:3-5 ).
Kinyume na asili ya Mungu ndiyo maana ya machukizo ( un contrallel to
his nature ). Machukizo kwa asili yalikuwa ni ya mataifa na hayakuwa ya
Waisraeli.
( YEREMIA 4:1 )
“Kama ukitaka kurudi, Ee Israeli, asema BWANA, utanirudia mimi; na kama
ukitaka kuyaondoa machukizo yako, yasiwe mbele ya macho yangu, ndipo
hutaondolewa”.
Kuna uwezekano mkubwa hata wakuu wa makuhani ( maaskofu ) kuruhusu
machukizo kuingia nyumbani mwa Mungu. Machukizo yakiingia madhara yake
ni makubwa kwa watu wa Mungu. Tunaona katika andiko hilo chini kuwa hata
uwezo au mkono wa Mungu wa kuponya unaondoka kwa w
( 2 NYAKATI 36:14-16 ).
“Na zaidi ya hayo wakuu wote wa makuhani, na watu, wakakosa mno
sawasawa na machukizo yote ya mataifa; wakainajisi nyumba ya BWANA
aliyoitakasa katika Yerusalemu. Naye BWANA, Mungu wa baba zao akatuma
kwao kwa mikono ya wajumbe wake, akiondoka mapema, na kutuma; kwa sababu
aliwahurumia watu wake, na makao yake; Lakini waliwadhihaki wajumbe wa
Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, hata
ilipozidi ghadhabu ya BWANA juu ya watu wake, hata kusiwe na kuponya”.
Miujiza ya Mungu ya uponyaji kama wakati wa Yesu na wakati wa mitume
haiwezi kuonekana dhahiri kwa watu wanaoruhusu machukizo kwa watu wa
Mungu na ndani maskan i(nyumbani) yake Mungu, Utakuta watu
wanashughulika na mapepo tu kila siku lakini miujiza ya vipofu kuona,
viziwi kusikia, viwete kutembea, mabubu kuongea, wenye kigugumizi
kuongea sawasawa, wenye makengeza kuponywa na kila namna ya miujiza
mingine kama nyakati za mitume havionekani. Mamlaka waliyokuwa nayo
mitue ya kumwambia kuwete ‘ Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama
uende ( MATENDO 3;6 )’. Mamlaka haiko leo kwa watumishi wengi sababu ni
kwamba wameruhusu machukizo nab ado tu wanaendelea kuyatetea kwa bidii
nyingi.
( YOHANA 2:13-17 )
Yesu Kristo alipokuta watu wamegeuza hekalu soko alichukizwa mno na
kitendo kile ndipo akaamua kupundua meza zao, na kuwaondoa wote hekaluni
kwa kutumia kikoto. Aliuliza, Yesu hakuyavumilia machukizo nyumbani mwa
baba yake.
Watumishi wa Mungu leo wanatakiwa kufuata msingi aliouweka BWANA YESU
na si kuyaacha machukizo eti kwa visingizio vya kulinda kundilisipungue,
hatuwasaidii washirika wetu. Tunapaswa kumwondoa mwovu miongoni mwetu
ili wengine wajifunze kukaa katika viwango vyote vya neno la Mungu.
( iv ). Wanawake wanapaswa kufunika kichwa wakiwa katika ibada.
Wanapaswa kufunika wakiwa kanisani, wanapofanya huduma yoyote ya kiroho
mfano, kuomba, kuhutubu au kuhubiri.
( 1 WAKORITHO 11:4-5,7,10,13
‘ Sheria inayomkataza mwanamume kumwomba Mungu akiwa amevaa kofia pia
inayomkataza kuvaa kofia kanisani hiyo hiyo ndiyo inayomtaka mwanamke
afunike kichwa kwa ajili ya Malaika. Wanaosema ilikuwa desturi za
Wakorintho hawayaelewi maandiko vizuri. Biblia inasema ‘ Imempasa mwamke
awe na dalili ya kumilikiwa kichwani kwa ajili ya Malaika”. Angalia
vizuri neno ‘ imempasa=lazima”. Hakuna Biblia ya Wakorintho pekee yao,
tukichambua Biblia hivyo sisi Watanzania hatutabaki na kitabu
chichote.Yote yaliyoandikwa, yaliandikwa kwa ajili yetu wote ( WARUMI
2;16 ), Mungu atayahukumu mataifa yote kwa injili hiyohiyo
Tukitaka kuziona nguvu za Mungu waziwazi lazima tuwe mbali na
machukizo ya aina yoyote. Mafuta ya Mungu yanakuwa juu ya mtu
anayechukia machukizo ( WAEBRANIA 1:9 ). Mtu ambaye anatetea machukizo
yaliyomo ndani ya maskani ya Mungu lakini akifanya miujiza au maajabu
lazima tujiulize ni nguvu ipi inatenda kazi hapo?. Mungu mwenyewe
anasema kuwa mahali penye machukizo, ukono wake wa kuponya hauwezi
kuwepo ( 2 NYAKATI 36:14-16 ), Pia hawezi kupakwa mafutaNA Mungu (
WAEBRANIA 1:9 ).
Nyakati hizi tulizonazo watu wengi hawapendi kuambiwa ukweli,
wanapenda kudanganywa. Paulo mtume alitabiri juu ya nyakati hizi jinsi
watu watakavyotafuta waliu wa kuwafundisha uongo na kuikataa kweli ya
neno la Mungu ( 2 timotheo 4:3-4). Hata wakati wa nabii Isaya walikuwepo
watu waliotafuta walimu wengine wa mbali na Isaya aliyehubiri kweli
yote. Walisema kuwa wanataka mafundisho laini yadanganyayo ( ISAYA
30;9-10 ).Kama tunataka kuishi na Mungu milele hatuna budi kutubu dhambi
zetu kwa kumaanisha kuziacha na kuwa tayari kuyafuata maagizo yote ya
Neno la Mungu ( ZABIRI 119:6 ). Tunasafisha njia zetu kwa kutii neno la
Mungu na siyo walimu wetu wanaotufariji tuendelee kufanya machukizo
mbele za Mungu ( ZABURI 119;9 ). Walimu wanaowatia moyo watu ili
waendelee kuvaa mapambo na suruali kwa wanawake wote ni wafariji wa
kutaabisha ( AYUBU 16:2 ).
Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni? Ni utakatifu (WAEBRANIA
12:14). Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO
WA YOHANA 21:27). Kinyonge ni kipi? Ni yule anayetenda dhambi. Huyu
ni mtu asiyefaa, ni mnyonge! Je, wewe ni mtakatifu? Jibu ni la!
Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni
mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa
kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata
rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13; YOHANA 14:6). Je, uko
tayari kutubu sasa ili upate rehema hii? Najua uko tayari. Basi
fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni; “Mungu Baba asante
kwa ujumbe huu. Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi. Sistahili
kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.
Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo. Bwana Yesu niwezeshe.
Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu. Amen”. Mpendwa msomaji
umekubaliwa kuingia mbinguni. Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka
siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa
linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI !!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment